Posts

Showing posts from September, 2020
Image
  Ivan Edmund kutoka kampuni ya dawa za binadamu ya Philips Pharmaceuticals Tanzania Ltd. akitoa dawa kwa mwananchi aliyekutwa na tatizo la  moyo  mara baada ya kupata matibabu wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika jana katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Katika maadhimisho hayo wananchi walipata bila malipo huduma za Upimaji,ushauri, matibabu ya moyo na rufaa ya moja kwa moja kwa wale waliokutwa na matatizo ya moyo yaliyohitaji matibabu ya kibingwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akitoa elimu ya jinsi gani unaweza kuepuka kupata magonjwa ya moyo kwa wananchi waliofika katika viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo wilya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani. Katika maadhimisho hayo wananchi walipata bila malipo huduma  za Upimaji,ushauri, matibabu ya moyo na rufaa ya moja kwa moja kwa wale wali...

UN yamuunga mkono Magufuli kutokomeza ukatili wa mwanamke Ikungi

Image
     Picha ya pamoja ya Mkuu wa mkoa wa Singida  Dk. Rehema Nchimbi(mwenye kilemba) na       wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo mara baada ya uzinduzi wa mradi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi(kulia) akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania, Zlatan Milisic baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi    Na John Mapepele, Ikungi  MKUU wa  Mkoa wa Singida Mhe, Dk. Rehema Nchimbi  leo amezindua  miongoni mwa miradi mikubwa iliyowahi kutekelezwa nchini, mradi wa  pamoja  baina ya Mashirika ya Kimataifa ya UN Women na UNFPA kupitia ufadhiri  wa  Shirika la KOICA wa Tuufikie usawa  wa jinsia kupitia kuwawezesha wanawake na wasichana utakaogharimu takribani bilioni 11.5 za kitanzania  ambao utatekelezwa  katika Wilaya ya Ikungi mkoani Singida na Msalala mkoani  Shinyanga katika kipindi cha  miaka mitatu k...